Social Icons

Wednesday 3 January 2018

MAELEKEZO YA BODI YA MIKOPO KWA WADAIWA AMBAO BADO HAWAJAAJIRIWA

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imewataka wanufaika wote wa mikopo ambao wanadaiwa na hawajaajiriwa bado, wafike katika ofisi za bodi hiyo zilizoko katika maeneo mbalimbali nchini ama kuwasiliana nao, ili wapewe maelekezo na utaratibu maalum wa namna ya kulipa mikopo yao.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Bodi ya Mikopo zilizoko Mwenge, Jijini Dar es Salaam, mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa elimu ya Juu (HESLB), Abdul-Razaq Badru ametoa wito kwa wale ambao bado hawajaanza kurejesha mikopo yao, hata kama bado hawajapata ajira maalumu, wafike katika ofisi za bodi maeneo mbalimbali nchini ili kupewa maelekezo na utaratibu wa namna ya kuanza kurejesja mikopo hiyo.

“Tunatoa wito kwa wale ambao kwa sababu fulani fulani walikuwa hawajaanza kulipa, walipe na wanakaribishwa kwenye ofisi zetu. Hata wale ambao hawako kwenye ajira maalum kuna utaratibu maalum tumewatengenezea. Wanaweza kuwasiliana na sisi katika mawasiliano yetu au wakaja ktika ofisi za Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Arusha, Zanzibar na kwingineko il tuwape maelekezo na utaratibu maalum wa kulipa.” amesema Mkurugenzi Badru

Aidha Mkurugenzi Badru amesisitiza kuwa Bodi itahakikisha kuwa inawashughulikia wale wote ambao bado hawajarejesha mikopo yao ili waweze kuirejesha ikiwemo kuwachukulia hatua za kisheria na kuwafikisha mahakamani.

“Mtu yeyote aliyekopa mkopo kwa ajili ya kusoma, njia pekee ya kisheria inayoweza kumfanya asilipe mkopo huu, ni labda awe amefariki. Lakini kama umekopa, uko hai, uko hapa nchini na hata ukienda nje, sisi ni lazima utalipa huo mkopo kwa gharama yoyote ile,” amesisitiza.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Urejeshaji wa Mikopo, Phidelis Joseph amewataka wale ambao tayari wameshaanza kurejesha madeni katika akaunti za benki za Bodi ya Mikopo, waweke maelezo yote katika ”pay-in-slip’ zao.

“Wale wanufaika ambao wanajitokeza na wanalipa kwenye zile ‘bank accounts’ zetu waweke ‘details’ zote. ‘Unapodeposit’ unatakiwa utoe taarifa kwa Bodi ya Mikopo kwamba nimeweka pesa. Lakini vie vile unapoiandika ile ‘slip’ yako uiandike vizuri..,” amesema Phidelis Joseph.

Vile vile amewataka wanufaika wa mikopo ambao wameshaanza kulipa, wafike katika ofisi za Bodi ya mikopo ama kutumia mitandao ya Bodi, kwaajili ya uhakiki.

No comments: