Social Icons

Wednesday 26 July 2017

NEWS ALERT: UDSM YASTUKIA MATAPELI WANAOWAHADAA WANAFUNZI WANAOOMBA UDAHILI

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.



Tumepata taarifa kwamba kuna matapeli wamekuwa wakiwahadaa wanafunzi wanaoomba udahili wa mwaka wa kwanza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kuwapa taratibu zisizo sahihi na kisha kuwaibia fedha zao. 

Tunaomba kuujulisha umma kwa ujumla kwamba udahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unafanywa kwa kupitia mfumo wa kompyuta katika mtandao maalumu unaopatikana katika tovuti iliyopo kwenye anuani: udsm.admission.ac.tz. Maelezo ya jinsi ya kuomba udahili pamoja na habari nyingine za udahili zinapatikana katika tovuti ya chuo yenye anuani: www.udsm.ac.tz

Maombi hayapokelewi kwa kujaza fomu. Pili, ada ya maombi ya udahili ni Shilingi 20,000/= tu ambazo zinalipwa kwa kutumia mitandao ya simu kwa kufuata maelekezo yaliyowekwa kwenye mfumo wa udahili. 

Tunatoa pole kwa waliopata usumbufu na tunasisitiza umuhimu wa kufuata taratibu zilizo rasmi katika zoezi zima la udahili.

Tunawatakia udahili mwema.

Imetolewa na Kurugenzi ya Shahada za Awali
Simu:       +255222410069

+255222410751

No comments: