Social Icons

Featured Posts

Friday, 28 July 2017

TCU YAWATOA HOFU WANAVYUO UDAHILI

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 

Imeandikwa na Jacquiline Ngoya na Mwani Aeshi
Ofisa Habari Mwandamizi, Edward Mkaku
TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imesema kuwa haitegemei kufutiwa udahili kwa wanafunzi kwa baadhi ya vyuo, kutawakosesha baadhi ya wanafunzi watarajiwa nafasi au kozi walizodhamiria kwenda kuzisoma.
Akizungumza kwenye Viwanja vya Maonesho, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari Mwandamizi, Edward Mkaku alisema TCU haitahusika na wanafunzi ambao watakosa vyuo kwa sababu kwa sasa wameratibu udahili na hivyo ni jukumu la mwanafunzi kutafuta chuo kulingana na ufaulu alionao.
“Hatutarajii mwanafunzi kukosa chuo, na pia kufutiwa udahili kwa baadhi ya vyuo siyo sababu ya wanafunzi kukosa nafasi kwenye vile vyuo vilivyopo,” alisema.
CHANZOP HABARI LEO

Thursday, 27 July 2017

TCU YAJIZATITI KUIMARISHA UBORA WA ELIMU VYUO VIKUU.

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. Na. Thobias Robert - MAELEZO

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) itaendelea kusimamia kwa umakini ubora wa elimu vyuo vikuu ili kuzalisha wasomi wenye tija kwa Taifa na kuongeza ufanisi, ubunifu, maadili pamoja na utendaji kazi uliotukuka kwa vijana wanaohitimu elimu ya vyuo vikuu nchini.

Hayo yamesema leo na Afisa Habari Mwandamizi wa TCU Edward Mkaku wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hii katika maonesho ya vyuo vikuu yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini, Dar es Salaam.

“Kwa sasa TCU tunaratibu udahili ambao unafanywa na vyuo vikuu vyenyewe, wakishamaliza kudahili majina yataletwa kwetu, na sisi tutapitia majina yote ili kuyahakiki kama yana vigezo vyote vya kujiunga na chuo husika. Tutashirikiana na Baraza la Mitihani na tukigundua kuna mtu amechomekewa kujiunga na chuo akiwa hana vigezo tutamuondoa,” amefafanua Mkaku.

Amesema kuwa tume hiyo itatembelea vyuo vyote nchini ili kufanya ukaguzi wa jina kwa jina kwa ajili ya kujiridhisha, na kama ikitokea hakuna kasoro yoyote basi mwanafunzi ataendelea na masomo.

Mkaku aliongeza kuwa, ingawa zoezi la udahili limerudishwa vyuoni lakini bado TCU ina mamlaka ya kusimamia ubora, mwenendo, mitaala pamoja na kozi zinazotolewa vyuoni ili kukuza na kuendeleza elimu bora kwa ajili ya kuinua Taifa hasa wakati huu ambapo Taifa linaelekea katika mapinduzi ya uchumi wa viwanda.

Aidha amewataka wahitimu wawe makini katika kuzisoma kozi na kuchagua ili kusiwepo na mkanganyiko na malalamiko yanayotokana na kukosea kuchagua au kupangiwa kozi ambayo mhitimu hakuomba.

Hapo nyuma zoezi la udahili wa vyuo vikuu lilikuwa likifanywa na TCU, lakini kutokana na kuwepo kwa malalamiko mengi ya wanafunzi ya kupangiwa vyuo au kozi ambazo hawakuzichagua ama kuzipenda, mapema mwaka huu Rais Dkt. John Pombe Magufuli alisitisha zoezi la udahili  kupitia TCU na kuagiza udahili kufanyika moja kwa moja vyuoni kuanzia mwaka wa masomo wa 2017/18.
 

SERIKALI YAPIGILIA MSUMARI UDAHILI

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 

 Imeandikwa na Waandishi Wetu
BAADHI ya vyuo vilivyosimamishwa kufanya udahili katika baadhi ya programu zake, vimebainisha kuwa vimeanza kuchukua hatua ya kuondoa dosari hizo, na viko tayari kufanyiwa uhakiki tena.
Hayo yamebainishwa jana kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam kwenye maonesho ya 12 ya Taasisi za Elimu ya Juu nchini yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja. Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Augustine (SAUT), Padri, Thadeus Mkamwa alikiri kuwa baadhi ya matawi ya chuo chake, yamesimamishiwa udahili katika baadhi ya programu zake, lakini ni kutokana na tatizo la mawasiliano baina ya chuo hicho na TCU.
“Ni kweli walituletea notisi ya siku 14 tujibu kuhusu upungufu waliobaini, tumewajibu mapema tu, lakini wakati tunasubiria matokeo, tukasikia kwenye vyombo vya habari kuwa, baadhi ya programu zetu zimesimamishwa zisifanyiwe udahili, lakini tunalifanyia kazi,” alisema Mkamwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wakuu wa Vyuo Vikuu nchini. Kwa upande wake, Ofisa Uhusiano wa Vyuo Vikuu vya Kanisa Katoliki, Atunus Simwambi, alikiri kuwa programu iliyosimamishiwa udahili ilikuwa kwa muda wa miaka mitatu angu ianzishwe haijawahi kuwa na wanafunzi na hivyo kutofundishwa chuoni hapo.
“Programu hii ilianzishwa kwa ajili ya watu wanaotakiwa kuwa mapadri au wanaokwenda kufanya kazi za utume katika maeneo mbalimbali. Kwa kuwa kuna mchakato wa kuunganisha chuo chetu na Chuo cha Filosofia cha Kibosho, tulitarajia programu hii itarejea,” alisema. Chuo hicho kimesitishiwa programu moja ya Bachelor of Arts in Philosophy with Ethics. Naye Makamu wa Chuo cha Waislamu cha Morogoro (MUM), Profesa Hamza Njozi, pamoja na kukiri kuwa katika baadhi ya programu zilizosimamishwa udahili zilikuwa na changamoto ya walimu, alieleza kuwa dosari hizo zimefanyiwa kazi kama ambavyo Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ilivyoagiza katika notisi yake ya siku 14.
Alisema chuo hicho kilipatiwa notisi ya siku hizo 14 inayoanzia Julai Mosi hadi 14, mwaka huu, kufanyia marekebisho dosari hizo, lakini hata baada ya kutoa majibu, walishtukia kupitia vyombo vya habari, kuwa programu hizo zimesimamishiwa udahili. Akizungumzia taarifa ya TCU, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Watoa Elimu Wasiotegemea Serikali Kusini mwa Jangwa la Sahara(CIEPSSA), Benjamin Nkonya alisema uamuzi huo wa serikali ni nzuri kwani una nia njema ya kurudisha heshima ya elimu nchini.
Nkonya alisema hatua hiyo inapaswa kuungwa mkono na wadau wa elimu nchini kwa sababu yapo baadhi ya mambo ambayo yamechangia kiwango cha elimu kushuka wakiwemo baadhi ya wasomi ambao wameonesha udhaifu kwenye utendaji wao. “Kwanza kabisa tunaona jinsi rais anavyokerwa na baadhi ya wasomi ambao wanavuruga nchi badala ya kuwa kioo, ameona hakuna mwelekeo nah ii inawezekana ikatokana na mfumo wa elimu ambao wakati mwingine baadhi ya shule au vyuo vimetoa elimu isiyokidhi, sasa tunapojisahihisha ni vizuri ili tuwe na mfumo thabiti kwa manufaa ya taifa,” alisema Nkonya.
Alisema kwa bahati nzuri sekta ya elimu nchini kwa sasa imepata mtu sahihi kwenye wizara hiyo inayoongozwa na Profesa Joyce Ndalichako ambaye hata wao wana imani ataendelea kuiboresha zaidi kwa sababu utendaji kazi wake unatambulika. “Profesa Ndalichako ni mtu makini, nakumbuka nilipokuwa Shirikisho la Wamiliki na Mameneja wa Shule na Vyuo Visivyo Vya Serikali (TAMANGSCO) zaidi ya miaka 10, Profesa Ndalichako alipokuwa NECTA, aliadhibu shule au vyuo vilivyokosea, na alitoa adhabu kali hata wakati mwingine kufutia matokeo shule nzima alipobaini udanganyifu, alifanya hivyo kulinda heshima ya elimu,” alisema Nkonya. Hivyo akashauri kuwa uamuzi uliofikiwa na serikali kupitia TCU ni uamuzi sahihi na kuvishauri vyuo husika kufuata maelekezo ili kuhakikisha kiwango cha elimu kitolewacho kina ubora unaotakiwa.
CHANZO HABARI LEO

Wednesday, 26 July 2017

UFAFANUZI WA TANGAZO LA AJIRA SEKTA YA AFYA

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. WIZARA YA AFYA YATANGAZA NAFASI 3152 ZA AJIRA

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 
 NEWS ALERT: UDSM YASTUKIA MATAPELI WANAOWAHADAA WANAFUNZI WANAOOMBA UDAHILI

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.Tumepata taarifa kwamba kuna matapeli wamekuwa wakiwahadaa wanafunzi wanaoomba udahili wa mwaka wa kwanza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kuwapa taratibu zisizo sahihi na kisha kuwaibia fedha zao. 

Tunaomba kuujulisha umma kwa ujumla kwamba udahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unafanywa kwa kupitia mfumo wa kompyuta katika mtandao maalumu unaopatikana katika tovuti iliyopo kwenye anuani: udsm.admission.ac.tz. Maelezo ya jinsi ya kuomba udahili pamoja na habari nyingine za udahili zinapatikana katika tovuti ya chuo yenye anuani: www.udsm.ac.tz

Maombi hayapokelewi kwa kujaza fomu. Pili, ada ya maombi ya udahili ni Shilingi 20,000/= tu ambazo zinalipwa kwa kutumia mitandao ya simu kwa kufuata maelekezo yaliyowekwa kwenye mfumo wa udahili. 

Tunatoa pole kwa waliopata usumbufu na tunasisitiza umuhimu wa kufuata taratibu zilizo rasmi katika zoezi zima la udahili.

Tunawatakia udahili mwema.

Imetolewa na Kurugenzi ya Shahada za Awali
Simu:       +255222410069

+255222410751

Tuesday, 25 July 2017

TCU YASITISHA UDAHILI KWA VYUO 19 KATIKA MWAKA WA MASOMO 2017/2018.

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.

Friday, 21 July 2017

UDAHILI WA WANAFUNZI WANAOTAKA KUJIUNGA VYUO VIKUU KUANZA JULAI 22, 2017

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. Na Lilian Lundo - MAELEZO.


Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) umeutangazia Umma kuwa kuanzia Julai 22 mwaka huu vyuo vyote vya elimu ya juu hapa nchini vitaanza kupokea maombi ya udahili kwa mwaka wa masomo  2017/2018.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Prof. Eleuther Mwageni (pichani) ameyasema hayo leo, Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya kuanza rasmi udahili kwa mwaka 2017/2018.
Prof. Mwageni amesema kuwa waombaji wanatakiwa kutuma maombi yao  kwenye vyuo husika na siyo tena TCU kama ilivyokuwa kwa mwaka jana na miaka mingine ya nyuma.
Aidha amesema kuwa waombaji wahakikishe wanaomba programu za masomo ambazo zimeidhinishwa na kutambuliwa na TCU na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).
"Tunavikumbusha vyuo kutangaza programu ambazo zimeidhinishwa na kutambuliwa na TCU na NACTE, ikiwa chuo kitatangaza programu ambazo  hazitambuliki na Tume, basi chuo husika kitachukuliwa hatua," amesema Prof. Mwageni.
Ameendelea kwa kusema kuwa, orodha ya programu hizo inapatikana katika tovuti ya TCU ( www.tcu.go.tz) ambapo programu hizo zimegawanywa katika makundi mawili yaani Kidato cha Sita na Diploma.
Vile vile, Prof. Mwageni amewataka waombaji watakao chaguliwa kwa zaidi ya chuo kimoja, kuthibitisha kwa wakati chuo watakachokwenda ili kutoa nafasi kwa waombaji wengine.
Waombaji wamehimizwa kusoma kwa makini mwongozo wa udahili kwa mwaka 2017/18 ambao unapatikana kwenye tovuti ya Tume.  
Aidha Tume inawakaribisha wadau wote kushiriki maonesho ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yatakayofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es Salaam kuanzia Jula 26 hadi 29 mwaka huu ambapo zaidi ya vyuo 80 vinatarajiwa kuwepo katika maonesho hayo.

Wednesday, 19 July 2017

WAZIRI UMMY MWALIMU APONGEZA WASICHANA WALIOFAULU MTIHANI WA KIDATO CHA SITA

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A. Mwalimu (Mb), anatoa pongezi za dhati, kwa wanafunzi wote waliofaulu mtihani wa kidato cha Sita kwa mwaka 2017, ambapo kiwango cha ufaulu wa matokeo ya kitaifa kimepanda kwa asilimia 0.59 ikilinganishwa na mwaka 2016, huku watoto wa kike wakiongoza kwa ubora mwaka huu.

Waziri Ummy amempongeza Sophia Juma wa shule ya Sekondari Mazinde juu (Tanga) kwa kushika nafasi ya kwanza, sanjari na Agatha Julius Ninga wa shule ya Wasichana Tabora ambaye ameshika nafasi ya pili kitaifa.

Kadhalika, Waziri Ummy amewapongeza wanafunzi wote wa kike kwa jitihada walizoonesha na kuweza kufaulu mitihani yao kwa kiwango cha asilimia 97.21 ya waliofanya mtihani; ikilinganishwa na asilimia 95.34 ya wavulana waliofaulu. Waziri ameeleza kufarijika na juhudi ya wanafunzi wa kike, kufuatia ufaulu wa daraja la kwanza hadi la tatu kupanda kwa asilimia 94.07 katika madaraja haya ikilinganishwa na wavulana waliofaulu kwa asilimia 93.49. Juhudi hizi sio za kubezwa, na ni ishara thabiti kuwa mtoto wa kike akipewa nafasi hakika anaweza.

Wizara inatambua ushirikiano wa walimu, wazazi, na jamii ambao wamewezesha kufikiwa kwa ubora wa ufaulu wa watoto wa kike. Juhudi zenu zimesaidia utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kutoa fursa sawa kwa watoto wa kike na wa kiume katika kupata haki ya elimu. Mhe.Ummy amewasa watoto wa kike wa shuleni mbalimbali nchini kutafakari matokeo ya mwaka huu ili kuwa chachu ya kujitambua na kujikinga na mimba shuleni. Kama wanafunzi wa kike watajitambua watasoma kwa ari kubwa kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla.

Niwatake watoto wote wa kike waelewe kuwa wamehitimu daraja moja, hata hivyo bado wanalojukumu la kujiendeleza zaidi katika taaluma mbalimbali kama njia ya kumwezesha mtoto wa kike na mwanamke kuchangia katika maendeleo ya taifa kwa umahiri mkubwa.

NAFASI ZA KAZI MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE ZANZIBAR

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 


Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar, ni taasisi ya Serikali  iliyoanzishwa kwa sheria namba 8 ya mwaka 2011. 

Mamlaka ya Viwanja vya Ndege inatangaza nafasi za Kazi katika maeneo yaliyoainishwa hapo chini, kwa wazanzibar wenye sifa zinazohitajika.

1. OFISA USALAMA DARAJA LA I I (AVIATION SECURITY OFFICER GRADE II)  Nafasi 10  Unguja
Sifa ya kuingia kazini
 
Mwenye Shahada ya Kwanza/Stashahada ya Juu au Stashahada ya Uzamili katika fani ya Mifumo ya Kompyuta (IT) au Sheria au Sayansi ya Jamii au Utawala au Menejimemti ya Rasilimaliwatu  kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). 

NAFASI ZA KAZI WIZARA YA ARDHI,MAJI, NISHATI NA MAZINGIRA

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. Tume ya Utumishi Serikalini Zanzibar inatangaza nafasi za kazi kwa ajili ya Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira kama ifuatavyo:-

1. Afisa Mipango Miji Daraja la II “Nafasi 3”

Sifa za Waombaji:

• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza ya Mipango Miji kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2. Mchumi Daraja la II “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:

• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Uchumi’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

3. Afisa Ardhi Daraja la II “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza ya Usimamizi Ardhi na Uthamini kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

4. Mchoraji Ramani Daraja la III “Nafasi 2”

Sifa za Waombaji:

• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya ‘Stashahada’ katika fani ya ‘Catographer’ au ‘Civil Engineer kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

5. Mtunza Ramani Daraja la III “Nafasi 2”

Sifa za Waombaji:

• Awe ni Mzanzibari
• Awe amehitimu elimu ya ‘Stashahada’ ya ‘Kumbukumbu’ au ‘Geography’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

6. Mkaguzi Eka Daraja la III “Nafasi 2”

Sifa za Waombaji:

• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya ‘Stashahada ya Kilimo’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

7. Afisa Tehama Daraja la II “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Teknolojia ya Habari’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Jinsi ya Kuomba:

• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-

KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-

a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.

f) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 21 Julai, 2017 wakati wa saa za kazi.

Tuesday, 18 July 2017

CHUO KIKUU KIPYA KUANZISHWA ILI KUUNGA MKONO JUHUDI ZA JPM KUZALISHA WATOA AJIRA.

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 


Na. Thobias Robert – MAELEZO.
Taasisi ya Kiislam ya the registered Trustees of Masjid Ridhwaa (RTMR), imedhamiria kuanzisha chuo Kikuu mahsusi kwaajili ya kuwaandaa vijana wa Kitanzania kujiajiri tofauti na ilivyo sasa kwa baadhi ya vyuo kuandaa wahitimu wanaotegemea kuajiriwa.
Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Leo, Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa Taasisi  hiyo, Alhaj Suleiman Seif Nassor, alisema lengo na dhumuni la taasisi yake ni kuanzisha Chuo Kikuu kitakachoendana na zama hizi za kidijitali za kuzalisha wataalam watakaoweza kujiajiri wenyewe kwa kutumia teknolojia zilizopo.
“Chuo Kikuu tunachotarajia kuanzisha kitatoa wahitimu ambao wao wenyewe watakuwa wenye kujiajiri na pia kutoa ajira tangu siku ya kwanza ya kuhitimu shahada zao,” alisema Mwenyekiti huyo.
Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa mifumo ya utoaji wa Elimu iliyopo katika Vyuo Vikuu  vingi hapa nchini, inamjenga mwanafunzi kuwa tegemezi wa serikali na mashirika binafsi ili yamuajiri lakini wao kama Taasisi yenye lengo la kuendana na sera ya serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya viwanda wana mpango wa kubadilisha mfumo na mtazamo huo.  
“Ili kuendana na sera za awamu hii, taasisi imetafakari kwa kina pamoja na kufanya tafiti mbalimbali na    kubaini kuwa ni lazima tubadili muundo wa utoaji shahada uliopo sasa wa kuandaa watafuta ajira,na badala yake tuandae wataalamu watakaojiajiri na kuajiri wenzao.
Shahada zinazotarajiwa kuanzishwa ili kuendana na halihalisi ya soko la sasa, pamoja na mabadiliko ya kisayansi na teknolojia nipamoja na BSc. Enterpreneur management, BSc. Agricultural Bussiness, Freelance Photo Journalism pamoja na Corporate communication.
Aidha kwa upande wa miundombinu Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa tayari walishaanza kujenga jengo la Chuo hicho lenye ghorofa tano  na amewaomba watanzania wenye kiu ya maendeleo kujitoa kwa hali na mali kuchangia ujenzi, ili kuunga mkono juhudi za Serikali za kuwakomboa watanzania katika lindi la umaskini.
Wakati huohuo Mwenyekiti huyo wa taasisi ya RTMR amepongeza juhudi zinazofanywa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kupambana na ubadhirifu wa mali za uuma pamoja na kuleta uwazi na uwajibikaji katika utumishi wa umma.
“Mh.Rais ameonyesha dhamira ya dhati kupambana na madawa ya kulevya ambayo yameathiri vijana wengi ambao ni nguvu kazi ya taifa, hivyo nasisitiza sisi kama viongozi wa dini na watanzania wote kwa ujumla tumuombee dua ili aweze kukamilisha ndoto yake ya kuifanya Tanzania kuwa nchi  yenye neema “ Alisema. 
Miongoni mwa shughuli za kimaendeleo zinazofanywa na taasisi ya RTMR ni pamoja na Kujenga misikiti, Vituo vya Afya, Vituo vya Elimu, pamoja na miradi ya kujikwamua kiuchumi kwa kuzingatia misingi ya kiislam.
Mwisho

 

Saturday, 15 July 2017

MPYA KABISA: Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2017 pamoja na Ualimu 2017 haya hapa

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 


Bofya Hapa Kutazama Matokeo ya Mtihani wa Kidato Cha Sita ACSEE mwaka 2017
Bofya Hapa Kutazama Matokeo ya Ualimu Ngazi ya DSEE mwaka 2017
Bofya Hapa Kutazama Matokeo ya Ualimu Ngazi ya GATCE mwaka 207