Social Icons

Wednesday 14 September 2016

HOT NEWS: Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu haihusiki kumtafutia mtu ajira

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255629914471. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 


Na Godfriend Mbuya
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu haihusiki kumtafutia mnufaika wa mkopo ajira badaya lake inahusika kumpatia mwanafunzi mkopo na akishamaliza muda wa masomo atatakiwa kurejesha mkopo wake.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na  Mkurugenzi Msaidizi wa Mawasiliano kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Cosmas Mwaisobwa wakati akijibu maswali ya wananchi kupitia mtandao wa Facebook.com/eatv.tv katika kipengele cha KIKAANGONI ambapo mgeni hufika EATV na kujibu maswali ya hadhira kulingana na mambo mbalimbali yanayohusu taasisi yake, au kazi yake.
“Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu inatoa mikopo suala la kutafuta ajira halituhusu hivyo mnufaika yoyote asiwe na kigezo kwamba hajapata kazi , hiyo siyo kazi yetu, kazi yetu ni kuwawezesha kupata elimu basi” Amesema Mwaisobwa.
Aidha Mwaisobwa amesema wanufaika wote ambao walipata mikopo wanatakiwa kukatwa asilimia 8% ya pato la mwezi, na kama mtu anagfanya kazi binafsi na hakatwi popote atatakiwa kutoa kiwango cha 120,000/=  na kwa ambao wamenufaika na hawataki kuanza kulipa mkopo watapigwa penati ya 10% ya mkopo kwa mwaka.
Pamoja na hayo Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu imewataka walioomba mikopo kuvuta subira kwani Bodi inasubiri majina kutoka Tume ya Vyuo Vikuu ili Bodi ya Mikopo iweze kufahamu vyuo walivyopangiwa na kiwango cha ada ili haki iweze kutendeka kwa waombaji.
 

No comments: