Social Icons

Thursday 11 February 2016

Wanafunzi SUA wataabika kwa kukosa mkopo

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 


Wanafunzi 204 wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine wapo hatarini kukwama kimasomo na kujikimu kimaisha baada ya kukosa mkopo kwa muda mrefu tokea mwezi Novemba hadi sasa mwezi wa pili 2016.


Akizungumza na waandishi wa habari chuoni hapo rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho Osca Ndunguru ametupia lawama bodi ya mikopo kuendelea kuwatesa wanafunzi huku wanafunzi hivyo amemuomba rais Magufuli kutembelea bodi ya mikopo kuchunguza uozo unaofanyika na kwamba bodi hiyo ihakikishe inashugulikia tatizo la wanafunzi hao ndani ya siku tatu.


Nao baadhi ya wanafunzi walioathiriwa na tatizo la kukosa mikopo wameeleza kusikitishwa kwao na kwamba wanalazimika kuishi kwa tabu kwa kukopeshana wanafunzi kwa wanafunzi wakitegemea bodi ya mikopo itawalipa fedha zao lakini kadri siku zinavyozidi kusonga mbele hali ya maisha yao chuoni yanazidi kuwa magumu.

Aidha waziri mkuu wa serikali hiyo ya wanafunzi amesisitiza na kuiomba serikali ya rais Magufuli kuangalia upya mfumo wa utendaji wa watumishi wa bodi ya mikopo kwani wanafanya kazi hiyo kwa mazoea na upendeleo kwa baadhi ya watu hali inayozorotesha maendeleo ya nchi.

No comments: