Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.
Na Jenikisa Ndile
Idadi ya wanafunzi
wanaopata mikopo kutoka Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa
Elimu ya Juu (HESLB) imekuwa imeongezeka mwaka hadi mwaka na kusaidia kuongeza
idadi ya watanzania wanaopata elimu ya juu.
Katika mwaka wa masomo wa 2005/2006
Bodi ya Mikopo ilitoa mikopo kwa
wanafunzi 42,729 iliyogharimu sh.
bilioni 56.1 na mwaka wa masomo
wa 2014/2015 bodi ya mikopo ilitoa mikopo kwa wanafunzi 98,000 iliyogharimu
shilingi bilioni 345.
Hayo yalisemawa leo na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano
kutoka bodi hiyo Cosmas Mwaisobwa wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa Idara ya
Habari (MAELEZO) kuhusu mafanikio ya
bodi hiyo katika kipindi hicho.
Alisema kwa kipindi hicho chote wamekuwa na sheria mbalimbali ilioanzishwa
kwa kuwapa jukumu la ukusanyaji wa madeni ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya
juu ambayo ilianza kutolewa tangu mwaka 1994/1995 kupitia iliyokuwa Wizara ya
Elimu,Sayansi na Teknolojia wakati huo Serikali haikukusanya madeni kutoka kwa
wanufaika hadi pale bodi ilipoanza kazi
rasmi mwaka 2006/2007.
Aliongeza kuwa taasisi hiyo
imekuwa na mafanikio makubwa
kulinganisha na hapo awali kwani kwa kipindi cha miaka kumi tumeongeza ufanisi
katika matumizi ya teknolojia ya habari
na mawasiliano (TEHAMA) kwa lengo la
kuomba mikopo kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa uombaji wa mikopo wa (OLAMS)
Aidha
bodi hiyo imeendelea kukua kwa
kasi kutokana na idadi ya watumishi kutoka tisa hadi kufikia watumishi 135
mwaka huu,ongezeko hilo limesaidia bodi kuwa na ufanisi katika utekelezaji wa
majukumu yake.
Bodi hiyo imewawezesha wateja wake kupata huduma katika maeneo manne ambayo
ni Arusha, Mwanza, Dodoma, na Zanzibar
ili kupata huduma za kibodi kwa ukaribu zaidi.
Mwaisongwa aliwahakikishia
wateja hao wataendelea kuwanufaisha waombaji na kutambua
kuwa mikopo ya wanafunzi wa elimu
ya juu ni sehemu ya utekelezaji wa sera
ya uchangiaji wa elimu ya juu na ni muhimu kurejesha mikopo ili kuwezesha mfuko
huo kuwa endelevu.
Taasisi hiyo iliyoanzishwa kwa mujibu
wa sheria namba 9 ya mwaka 2004 na
kuanza rasmi julai 2005 yenye lengo la kutoa mikopo kwa wanafunzi i wa elimu ya
juu,utoaji na ukusanyaji wa mikopo ili kufanya mfuko wa mikopo kuwa endelevu.
No comments:
Post a Comment