Social Icons

Thursday 24 July 2014

KARDINALI PENGO AWAPONGEZA WALIOFANYA VIZURI MITIHANI YA KIDATO CHA SITA 2014

 

Kufuatia kufanya vizuri kwa Shule ya Sekondari ya St. Joseph ya Jijini Dar es Salaam ambayo inamilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam,  Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo Julai 18, mwaka huu alikutana na wanafunzi wa tatu walioongoza Kitaifa na kuongoza kwa masomo na kuwapa pongezi.

Pichani juu ni Muadhama Polycarp Kardinali Pengo, akisalimiana na wanafunzi waliofanya vizuri kitaifa kutoka shule ya Sekondari ya  St. Joseph Cathedral ya Dar es Salaam ambayo inamilikiwa na Kanisa Katoliki ambao ni , Joseph Ngobya wa masomo ya Sanaa na Lugha, Isaack Shayo aliyeshika namba moja kitaifa (katikati) na Prince Mwambaja (wapili kushoto) aliyeshika nafasi ya tano kitaifa masomo ya biashara.
 Mwalimu Mkuu,Sr. Theodora Faustine akizungumza wakati wa mkutano huo.
 Wazazi walimpa Kardinali zawadi kwa kuanzisha shule hiyo na kutoa elimu kwa vijana wao.
 Sr. Theodora Faustine ambaye ndio Mkuu wa shule ya Sekondari ya  St. Joseph Cathedral akizungumza.
 Wanafunzi wakiwa katika Mkutano huo wa shukrani kwa Kardinali Pengo.
 Picha ya pamoja kati ya wahitimu na Kardinali Pengo na familia ilipigwa.
 Wahitimu wakizungumza yao.
Wahitimu wakiwa na mwalimu wao Mkuu, Sr. Theodora Faustine. 
Kwa hisani ya Father Kidevu Blog
Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.

No comments: