Social Icons

Friday 25 July 2014

HOT NEWS: MAHAKAMA YA KANDA YA MBEYA IMEENDELEA KUSIKILIZA KESI INAYOWAKABILI ASKARI WATATU WA JESHI LA POLISI WANAODAIWA KUMUUA MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA TEKU


Marehemu Daniel Godluck Mwakyusa (31) ambaye ni mwanafunzi wa chuo cha TEKU aliyeuawa na Askari wa Jeshi la Polisi PC Maduhu tarehe 14/02/2012 katika sikukuu ya wapendanao [valentine day].
**** 

Na mwandishi wetu- Matukio na wanavyuo
Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya imeendelea kusikiliza kesi  ya mauaji inayowakabili Askari watatu wa Jeshi la Polisi wanaodaiwa kumuua Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha TEKU Daniel Mwakyusa Februari 14 mwaka 2012.

Kesi hiyo inasikilizwa na Jaji Rose Temba wa Mahakama Kuu aliyekuja maalum kusikiliza kesi hiyo baada ya upelelezi kukamilika ambapo imeanza kusikilizwa mfululizo Julai 21 mwaka huu.

Wanaotuhumiwa katika kesi hiyo ni pamoja na F 5842 DC Maduhu,E 7769 DC Shaban na WP 6545 DC Neema ambao wanatetewa na Wakili wa kujitegemea Mika Thadayo Mbise na wamekana shitaka hilo.

Wakili wa Serikali Hashim Ngole ameiambia Mahakama kuwa kosa hilo ni kinyume cha sheria ya makosa ya jinai namba 196 sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 na kwamba Askari hao wakiwa doria walimuua mwanafunzi huyo baada ya kumkamata ukumbi wa Univesal Pub.

Upande wa mashitaka umeleta mashahidi 11 na shahidi wa mwisho katika kesi hiyo alikuwa rafiki wa marehemu David Lisbon(24)ambaye aliiambia Mahakama kuwa walikuwa wametoka na marehemu kwenda matembezini Univesal Pub majira ya saa mbili usiku na walipitia eneo jingine kabla ya kuingia Univesal Pub saa nne usiku.

Baada ya kusililiza mashahidi upande wa mashitaka ambao umefunga ushahidi wake Jaji Temba akisaidiwa na wazee watatu washauri alisema kuwa washitakiwa wote watatu wanayo kesi ya kujibu hivyo wataanza kujitetea leo tarehe 25 mwaka huu.
Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.

No comments: