Social Icons

imetosha

imetosha

Featured Posts

Monday, 13 April 2015

Serikali yaombwa ruzuku vyuo binafsi vya uuguzi, ukunga.


Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid.
Serikali  imeshauriwa kutoa ruzuku kwa vyuo vya uuguzi na ukunga vinavyomilikiwa na watu binafsi, ili kuongeza idadi ya 
wataalamu wa kada hiyo kwa lengo la kupunguza ama kumaliza vifo vya mama na mtoto.
 
Wito huo ulitolewa na Mkurugenzi wa Chuo cha Uuguzi na Ukunga Profesa Richard Lema, kwenye mahafali ya saba ya stashahada na ya pili ya cheti kwa wahitimu wa uuguzi na ukunga toka chuo cha Massana, jijini Dar es Salaam.
 
Profesa Lema alisema iwapo vyuo binafsi vitapatiwa ruzuku na serikali kama inavyofanyika kwa vyuo vyinavyomilikiwa na misheni, kada ya uuguzi na ukunga itapata watumishi wengi, hivyo kuisadia serikali katika kupunguza vifo vya akina mama na watoto nchini.
 
“Ni dhahiri hatuwezi kupunguza vifo vya akina mama na watoto bila ya wakunga wa kutosha kwani hawa ndio wadau muhimu wa kupunguza vifo vya akina mama na vitoto vichanga, na muhimili wa kutekeleza malengo ya namba nne na tano ya Milenia,” alisema.
 
Alisema tatizo linalovikumba vyuo vya ukunga na uuguzi vya watu binafsi kama hicho cha Massana, ni lile la wanafunzi wa fani hiyo kushindwa kuendelea kutokana na tatizo la ada, pale wafadhili wao wanapojitoa kutokana na sababu mbalimbali.
 
Alisema tatizo hilo linaweza kutatuliwa na serikali kwa njia tofauti, ikiwa ni pamoja na kuwaingiza walimu wa vyuo binafsi vya uuguzi na ukunga kwenye mpango wa mkataba na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
 
 “Na hili linawezekana tukiwa kama wadau wa serikali, kwa sababu wahitimu wetu huajiriwa na wizara na kupangiwa kufanya kazi katika maeneo karibu yote nchini,” alisema.
 
Naye mgeni rasmi katika mahafali hayo, Profesa Paulina Meela, aliwataka wahitimu hao wakafanye kazi kwa kuzingatia miiko na maadili kama walivyofundishwa.
 
Jumla ya wanafunzi 23 wa Stashahada ya uuguzi na ukunga inayochukua miaka mitatu na wanafunzi 17 wa cheti cha miaka miwili, walihitimu mafunzo hayo.
 
CHANZO: NIPASHE

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.

Wednesday, 1 April 2015

HOT NEWS: MWANDOSYA AWAVURUGA VIONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYUO VIKUU MBEYA. Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyuo vikuu Mkoa wa Mbeya(CCM),Raymond Mweli akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakikanusha kuhusu wenzao kutumia jina la shirikisho hilo kumshawishi Mwandosya kugombea urais
 Katibu Shirikisho la Vyuo vikuu Mkoa wa Mbeya(CCM),Karimu Nyanga akisoma tamko kuhusu wenzao kutumia jina la shirikisho hilo kumshawishi Mwandosya kugombea urais.
 Baadhi ya viongozi wa Shirikisho wakiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari.
 Baadhi ya Waandishi wa habari wakichukua maelezo kutoka kwa viongozi wa shirikisho.

SHIRIKISHO la Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) mkoani Mbeya limeonekana kuwa na mkanganyiko juu ya tamko lililotolewa na baadhi ya wanashirikisho hilo la kumtaka mbunge wa Rungwe Mashariki Prof.Mark Mwandosya kugombea urais.

Mkanganyiko huo umekuja baada ya matamko mawili kutolewa kwa siku tofauti na wanashirikisho hilo,moja likimtaka Prof Mwandosya kuchukua fomu na jingine likilaani tamko la awali kuwa lilikuwa batili.

Tamko lililotolewa  na katibu wa jumuiya hiyo Karimu Nyanga kwa wanahabari lilibainisha kuwa tamko la tarehe Machi 21 la kumtaka Prof Mwandosya kuwania urais halikutolewa na uongozi wa jumuiya kama watoa tamko hilo walivyobainisha.

Nyanga alisema waliotoa tamko hilo walikuwa watu wachache wasio na nia njema juu ya shirikisho,Chama na taifa kwa ujumla,

“Kimsingi tumesikitishwa sana na kuhuzunishwa sana juu ya matamko hayo ambayo yapo kinyume na misingi ya kimaadili ya chama cha mapinduzi licha ya ukweli kwamba watu hawa si viongozi wala hawakuwahi kuwa viongozi wa shirikisho la vyuo vikuu mkoa wa Mbeya.Tunashangazwa na matamko yasiyo na tija kwa shirikisho na kwa chama yaliyotolewa na watu ambao si viongozi wa shirikisho letu” alisema Nyanga.

Alisema msimamo wa shirikisho hilo ni kutofungamana na upande wowote wa urais kwa sasa wakiamini kwamba wakati muafaka ukifika vikao halali vya chama vitawaletea mgombea wa urais anayetosha kupeperusha bendera ya chama chao katika uchaguzi mkuu ujao.

Mnamo Machi 21 mwaka huu watu waliojiita viongozi wa shirikisho hilo mbelea ya wanahabari walitoa tamko la kumtaka Prof Mwandosya kuchukua fomu ya kuwania urais wakisema ana sifa za kuwania nafasi hiyo.

Akisoma tamko hilo Oscar Mwaihabi aliyejitambulisha kama katibu wa shirikisho alisema kwa pamoja wanashirikisho wamekubaliana kumshawishi Prof Mwandosya baada ya kuridhishwa na sifa alizo nazo.


Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.

Monday, 30 March 2015

WANAFUNZI WA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA(TPSC) TAWI LATANGA WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO PSPTB


1
Wageni wakiwasili kwenye ofisi za Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi.
New Picture (3)
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa PSPTB, Dr Tesha akitoa hutuba ya ufunguzi kuwakaribisha wanachuo wa mwaka wa pili wa stashahada ya Ununuzi na Ugavi kutoka chuo cha TPSC Utumishi wa Umma tawi la Tanga.
New Picture (4)
Wanachuo wakimsiliza Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Bodi Dr. Tesha.
New Picture (5)
Mkurugenzi ya Mafunzo, Bw. Godfred Mbanyi akielezea juu ya madaraja ya mitihani ya Bodi na taratibu za kufanya mitihani.
New Picture (7)
Bw. Ally Songoro kutoka Kurugenzi ya Taaluma akifafanua jambo, juu ya taratibu za usajili, miiko ya wanataaluma kwa wanachuo waliotembelea Bodi.
New Picture (9)
Bw. Paul Bilabaye kutoka Kurugenzi ya Fedha na Utawala akielezea taratibu za malipo ya huduma mbalimbili zitolewazo na Bodi.
New Picture (10)
Mwanachuo mmoja akiuluza maswali juu ya kazi mbalimbali za Bodi Wataalam wa Ununuzi na Ugavi.
New Picture (11)
Mmoja wa wanachuo akiuliza maswali juu ya kazi mbalimbali za Bodi Wataalam wa Ununuzi na Ugavi.
New Picture (1)
Wanachuo wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye ofisi za Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi.
New Picture (2)
Baadhi ya wanafunzi kwenye picha ya pomoja pamoja na mkurugenzi Mkurugenzi mtendaji wa Bodi Dr. Clemence Tesha na viongozi waandamizi wa Bodi.
.....................................................................
Na Mwandishi wetu
Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imepokea ugeni wa wanachuo sabini wa mwaka wa pili wanaosoma stashahada ya ununuzi na ugavi waliokuja kwenye ziara ya mafunzo kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la Tanga. Ziara hiyo ya mafunzo ililenga kujua kazi mbalimbali za Bodi ya wataalam wa ununuzi na Ugavi (PSPTB). Mkurugenzi mkuu Mtendaji wa PSPTB Dr Clemence Tesha, aliupokea ugeni huo, na kuwashukuru kwa kuona nia ya kufanya ziara ya mafunzo. Aidha aliwaelezea umuhimu wa kuzingatia maadili , kujifunza kwa bidii ili kupata maarifa na ujuzi unaoweza kuhimili soko la ushindani la ajira . Wanachuo pia walielezewa juu ya taratibu za mitihani ya Bodi yenye ngazi ya cheti cha awaliAwali, msingi Msingi na Taaluma. Aidha aliwaelezea taratibu za kusajii kwa ajili ya kufanya mitihani ya kitaaluma mara baada ya kumaliza masomo yao na kwamba mhitimu wa stashahada ya ununuzi na ugavi kwa chuo kinachotambuliwa na Bodi anaanzia ngazi ya kwanza ya mitihani ya taaluma. Mitihani ya taaluma ina ngazi tano, ambazo huhitimishwa kwa wanafunzi kufanya mitihaniutafiti. Ziara hiyo pia ilitoa fursa kwa wanachuo hao kujua taratibu za kujisajili kama wataalum wataalam wa Ununuzi na Ugavi kwani ni hitaji la sheria iliyounda Bodi. Aidha walifahamishawa kwamba kuna ngazi mbalimbali za usajili ambazo zinatambua kiwango cha ujuzi na uzoefu wa mtaalam. “ fanyeni usajili mara mmalizapo chuo ili kutumia fursa za ajira katika fani yenu “ ” alisisitiza. Tambueni kwamba taaluma ya ununuzi na ugavi inaongozwa na misingi ya maadili ambayo inawataka kutambua kuwa mnawajibika kwa umma wa watanzania, taaluama yenu, mwajili wako. Misingi hii ya wajibu ndio inayoifanya taaluma hii iwe ya kipekee. “maadili huanzia 

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.

MADEREVA 21 WA KAMPUNI YA MAJINJAH LOGISTICS LTD WAPATIWA MAFUNZO CHUO CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI (NIT) WAHITIMU WAPEWA VYETI.‏


 Wafanyakazi wa Kampuni ya Majinjah Logistics Ltd wakiwa katika picha ya pamoja na kutoka kushoto mstari wa mbele (wa pili) Mkuu wa Kampuni ya Majinjah,Geoffrey Mwambona, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Majinjah Logistics,Benjamin Mwandete,Mkuu wa Idara ya Tafiti,Machapisho na Masomo ya Elimu ya Juu (NIT),Dk,Ethel Kasembe,Mhandisi, Charles Kisunga na Dereva wa kike wa Majinjah,Grace Andrew.
 Wahitimu wa mafunzo ya Udereva wa Kampuni ya Majinjah Logistics wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wao na viongozi wa NIT.


  Mhandisi, Charles Kisunga wa NIT akizungumza,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Majinjah Logistics,Benjamin Mwandete (kushoto) Mkuu wa Idara ya Tafiti,Machapisho na Masomo ya Elimu ya Juu (NIT),Dk,Ethel Kasembe (wa pili kulia) na Mkuu wa Kampuni ya Majinjah,Geoffrey Mwambona,
 Mkuu wa Idara ya Tafiti,Machapisho na Masomo ya Elimu ya Juu,Dk,Ethel Kasembe (kulia) akizungumza kabla ya kukabidhi vyeti wahitimu.Wengine ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Majinjah Logistics,Benjamin Mwandete na Mhandisi, Charles Kisunga wa NIT.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Majinjah Logistics,Benjamin Mwandete (kushoto) akitoa nasaha kwa wahitimu.Mwalimu wa Madereva, Daniel Kasisi,akifuatilia utoaji wa Vyeti kwa Wahitimu 21 wa Maginjah Logistics Ltd. 
Na Mwandishi Wetu
Madereva 21 wa Kampuni ya Majinjah Logistics Ltd wamepatiwa mafunzo ya siku tatu katika Chuo cha Taifa cha Usafirishji (NIT).

Mafunzo hayo yalihusu Alama na Michoro ya barabarani,Sheria,Udereva wa Kujihami,Vyanzo vya Ajali jinsi ya kuzizuia,Huduma kwa Wateja na mawasiliano ya Barabarani.

 Mkuu wa Idara ya Tafiti,Machapisho na Masomo ya Elimu ya Juu,Dk,Ethel Kasembe,aliwaambia madereva kuwa elimu waliyoipata itawasaidia kuepusha ajali za barabarani wakati wakiendesha mabasi yanayobeba abiria na kuwataka waendelee kupata elimu ya kutosha.
Alisema kuwa imani yake takwimu za ajali zitapungua na hata kwisha kabisa kama watazingatia waliyofundishwa na kuwasisitiza kwenda Chuoni hapo mara kwa mara kuendelea  kupata elimu.

Pia alisisitiza kuwa watabadilika baada ya kumaliza mafunzo ya hapo na kuwa vyanzo vya ajali watavizuia kwa kutumia udereva wa kujihami wakiwa barabarani wakati wote.
Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.

Thursday, 26 March 2015

WANAFUNZI WA CHUO CHA UTUMISHI WA UMA MBEYA MAFUNZONI BUNGENI DODOMA HII LEO


WANAFUNZI 97 kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma, Tawi la Mbeya, leo wapo Bungeni mjini Dodoma kwa ziara ya kimafunzo. Wanafunzi hao wanaosomea fani mbalimbali zikiwepo utunzaji kumbukumbu na makatibu Muktasi watajifunza vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujioenea moja kwa moja namna shughuli za Bunge zinavyofanyika. 
Wanafunzi wakifuatilia mjadala kwa umakini.
Mhadhiri na Kiongozi wa Chuo hicho, Johnson Mbuluma (kulia) akiwa na wanafunzi wake wakifuatilia shughuli mbalimbali za Bunge mjini Dodoma hii leo.
Wanafunzi hao wakiwa Bungeni wakifuatilia mijadala hiyo mbalimbali na kipindi cha maswali na majibu.

Wanafunzi mbalimbali hutembelea Bungeni kwa ajili ya mafunzo na pia makundi mbalimbali katika Jamii. Father Kidevu

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.